Loading...

CCM NA CHADEMA WAGOMBEA WAO WAKIMBILIA MITINI (MDAHALO)


Siyo jambo la kushangaza kuona vinara wa vyama viwili CHADEMA na CCM wagombea wao wao

wakimbilia mstuni. Kama ni mfuatilija wa siasa za Tanzania ili siyo jambo la Ajabu Sana kwani hata

chama/vyama fulani vilikimbilia mitini wakati wa HARAKATI MAJIMBONI 2010. Watanzania

tujifunze kwamba wanasiasa wetu siyo wakweli. Wengine walipromise tena kwa kujigamba

majukwaani wakiahidi kwa kujigamba wagombea wao wako tayari kwa midaharo. Makada hawa pia

walionekana katika Runinga na Vyombo Vingine vya habari wakipiga propaganda hizi, tena kwa

madaha na majigambo. Kweli waswahili usema maneno matupu hayavunji mfupa, na palipo na

ukweliuongo hujitenga hili limejitokeza tena. Kwa kumbukumbu zangu za mwaka 2010 ziliwafanya

watu fulani fulani ajira zao kukoma. Je huo ndio uzalendo na uadlifu na

uchapakazi,............................ UTAJAZA MWENYEW!!!!!!

                                                     Tanzania

MKE Alininyanyasa Sana Nilipofukuzwa Kazi, MUNGU Ameniona, Sasa Yamegeuka

Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.

Kama humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.

Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-

(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.

(2) Chake kikawa chake tu.

(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.

(4) Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.

(5) Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.

Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.

(6) Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing. Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa amepotezea moja kwa moja.

Hata wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele, maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia, huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.

Baadae akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani, nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi ya salam za asubuhi na jioni tu basi.

Wana jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.

Nimeanza mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na matarajio yangu wife kwa kuwa alishaƱichoka na hakuna kinachoendelea kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele

Wakuu sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.


NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo

Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo

Naomba ushauri wenu

UKAWA/CHADEMA: RATIBA YA MGOMBEA URAISMH. E. LOWASSA


MREMBO Amtambia Mrembo Mwenzako: LUNGI Amlipua Agness Masogange.

MSANII wa siku nyingi kwenye anga la filamu Bongo, Lungi Maulanga amemlipua Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kwamba hajui kutumia umbo lake vizuri ndiyo maana amemtelekeza mwanaye.Akipiga stori na Ijumaa, Lungi alidai Masogange amemwacha mwanaye kwa shangazi yake huku malezi yake yakiwa duni wakati yeye akijiachia kimjini.

Masogange ananichefua kwa kuwa amemtelekeza mwanaye, mimi nina watoto watatu na ninahakikisha wanasoma shule nzuri sasa yeye huyo mtoto mmoja tu anamshinda, anamsomesha shule za kayumba, inakuja kweli hiyo?
“Halafu Mungu amemjalia kuwa na umbo zuri, sasa angekuwa analitumia vizuri angeshindwa kumlea mwanaye katika mazingira mazuri mpaka akamwache kwa shangazi wake. Mbaya zaidi hata gari zuri hana, sasa umbo lake linamsaidia nini?” alisema Lungi.

Baada ya paparazi wetu kumsomea mashtaka Masogange, mrembo huyo alisema: “Mwanangu nilimpeleka kwa baba yake, kama ingekuwa nimemwacha kwa marafiki au sehemu nyingine hapo ningeambiwa nimemtelekeza, kuhusu mafanikio yangu siwezi kutangaza kwamba nina hiki au kile.

Gari ni kitu cha kawaida sana, kitu cha maana ni nyumba sasa siwezi kuanika mambo yangu. Kuhusu umbo zuri huyo dada alitaka nijiuze? Siwezi kufanya biashara chafu mimi.”

Pigo Tena kwa CCM. Filikunjombe hatuna naye Nchini, Mola Amrehem, Amen!

si makao makuu Tanzania yathibitisha kifo cha mgombea wa CCM jimbo la Ludewa Iringa Bwana Deo Filikujombe kilichotokea maeneo ya hifadhi ya bunga ya Selou iliyoko mkoani Lindi na Pwani. Habari kamili na EATV


Lori laanguka na kuziba barabara muhimu Nairobi

  • Saa 6 zilizopita
 Ajali
Image caption Barabara ya Uhuru Highway hutumiwa kuingia jiji la Nairobi ukitokea upande wa Westlands
Msongamano mkubwa wa magari umeshuhudiwa katika moja ya barabara kuu za kuingia jiji la Nairobi baada ya lori kuanguka na kufuziba upande mmoja wa barabara.
Wengi wa wakazi waliokuwa wakijiandaa kwenda kazini kutumia barabara hiyo ya Uhuru Highway karibu wamelazimika kutumia muda mwingi kufika jijini.
Ajali hiyo ilitokea usiku mita chache baada ya kupita mzunguko wa barabara wa Museum Hill ukielekea Nairobi.
 Ajali
 
Lori hilo lilikuwa limebeba mahindi
Magari yanayotaka kuingia jijini yanaelekezwa kutumia barabara ya Kijabe Street, mwandishi wa BBC Bashkas Jugsoday anasema.
Eneo hilo liko karibu na chuo kikuu cha Nairobi.


   Foleni ndefu ya magari imeshuhudiwa katika barabara hiyo 
  Ajali
Hakuna ripoti zozote za majeruhi.
Barabara hiyo hutumiwa na watu wanaotoka maeneo ya magharibi mwa jiji na pia magharibi mwa nchi kama vile Naivasha na Nakuru, Eldoret na Kisumu.

Faini ya FA ni fedheha asema Mourinho

Faini ya FA ni fedheha asema Mourinho

  • 16 Oktoba 2015
 
Image copyright PA
Image caption Kocha wa Chelsea,Jose Mourinho
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema faini ya pauni 50,000 aliyotozwa na chama cha soka cha England (FA) ni fedheha.
Mourinho amepewa adhabu hiyo ya faini pamoja na marufuku ya mechi moja, ambayo haitatekelezwa kwa sasa, baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kufuatia kauli yake kuhusu refa Robert Madley mara baada ya Chelsea kufungwa 3-1 na Southampton.
Mourinho ameeleza kuwa kutozwa faini hiyo na kufungiwa mechi moja ni kitu cha kushangaza.
Mourinho pia alimchimba Meneja wa Arsenal Arsene Wenger bila kumtaja jina alipogusia kuwa Wenger, "alisema nini mara baada ya kuchapwa 2-0 na Chelsea Mwezi uliopita?".
Wenger alidai refa wa mchezo ule Mike Dean, alikuwa ‘dhaifu’ na ‘asiyefahamu’ soka.
Mbali na hilo, Wenger pia hakuadhibiwa na FA Oktoba 2014 wakati alipomsukuma Mourinho, aliyekuwa eneo lake la ufundi, Chelsea ilipopambana na Arsenal.
Older Posts
© Copyright shezzy taifa kubwa | Designed By Hisia za Mwananchi
Back To Top