Hii Hapa Taarifa Kutoka NEC Kuhusu Mashine za BVR Zilizosemekana Kukamatwa Katika Kiwanda cha MM Steel Zikiandikisha Watu
Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa mashine za kuandisha kwa njia za
kielekroniki zilizokamatwa katika kiwanda cha MM Steel, Mwenge, jijini
Dar es Salaam sio mashine za BVR kama ilivyodaiwa awali.
Mkurugenzi wa
NEC, Ramadhani Kailima amesema kuwa baada ya kuzifanyia uchunguzi
mashine hizo, wamebaini kuwa mashine hizo ni ‘feki’ na hazifanani na
mashine zilizotumiwa na Tume hiyo.
“Hakuna
ukweli wowote kwamba zile ni mashine za BVR na tumebaini ni feki. Tena
ni sawa na zile zinazotumika kwenye ofisi mbalimbali kuandikisha
wafanyakazi wake. Hao waliosema ni mashine za kuandikisha wapiga kura
hawako sahihi, sio kweli,” alisema Kailima.
Kailima
alieleza kuwa walifanya uchunguzi wa mashine hizo wakiwa pamoja na
baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa kwa kuwa wao
ndio waliiopeleka malalamiko kuhusu uwepo wa mashine hizo.
Mashine hizo
zilikamatwa juzi baada ya kuhisiwa kuwa na uhusiano na mashine za BVR
kwa kutokana na mfanano wake na njia zilizokuwa zinatumika kuwaandikisha
wafanyakazi kiwandani hapo. Mashine hizo tayari zilikuwa zimeandikisha
wafanyakazi 100.






Post a Comment